PaGo hutumia jina, simu, email na taarifa za safari/mizigo ili kutoa huduma, kuthibitisha akaunti na kutuma taarifa za huduma. Tarehe ya kuzaliwa ni ya hiari.
Kampuni iliyochaguliwa hupata taarifa zinazohitajika kwa huduma yake. Agent hutumia ruhusa za kampuni na ofisi aliyopewa. Rekodi za huduma za kampuni nyingine hazionyeshwi kwenye eneo lake la kazi.
SMS ndiyo njia ya msingi ya taarifa za huduma na OTP; email hutumika inapowekwa. WhatsApp ya tiketi hutumika ukichagua kuipokea na huduma ikiwa imewezeshwa. Kukubaliwa kwa ujumbe na provider hakumaanishi umefika kwa mpokeaji.
Ujumbe wa siku ya kuzaliwa na sikukuu ni wa hiari. Unaweza kuzima ujumbe huu kwenye Akaunti yangu wakati wowote bila kuzima OTP au taarifa za safari.
Unaweza kubadilisha taarifa kwenye Akaunti yangu na kuomba kufuta akaunti. Baada ya kukagua huduma, salio, madai na malipo yanayosubiri, profile ya login huondolewa na akaunti hufungwa. Rekodi za tiketi, malipo na custody ya mizigo huhifadhiwa kwa ufuatiliaji wa huduma na ukaguzi; taarifa binafsi zilizomo kwenye rekodi hizo huhitaji ukaguzi tofauti wa msimamizi.